Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la serikali ya Syria limekubali mpango wa usitishaji mapigano wa siku mbili katika mji wa Aleppo uliyoharibiwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekni.
Hatua hiyo imekuja baada ya Washington kutangaza kuwa Marekani na Urusi zimekubaliana kuzishinikiza pande hasimu kurefusha usitishaji huo usiothabiti. "Uongozi wa juu wa jeshi la Syria unatangaza kipindi cha utulivu mjini Aleppo kwa saa 48 kuanzia saa saba usiku wa kuamkia Alhamisi," ilitanza televisheni ya taifa ya Syria.
Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema wasimamizi wake wa mapatano ya kusitisha mapigano walikubaliana na wenzao wa Marekani kusimamia mapatano hayo hadi saa sita usiku wa Mei 4. Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alisema mapatano mapya ya Aleppo yalianza tayari usiku wa manane siku ya Jumanne, na kwamba vurugu tayari zilikuwa zimeshapungua.
Lakini waandishi wa habari walioko ndani ya Syria wameripoti kuendelea kwa mapigano makali ndani ya mji huo na maeneo yalioko magahribi mwa Damascus ambayo yalikuwa tayari chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Marekani inaunga mkono upande wa magaidi na Urusi inaunga mkono upande wa serikali ya Syria.
Ujumbe kwa serikali na wapinzani
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mark toner alisema kumekuwepo na kupungua kwa vurugu kwa ujumla, ingawa bado kulikuwa na ripoti za kuendelea kwa mapigano katika baadhi ya maeneo. Alizitaka pande mbili kuchukuwa hatua zinazostahiki.
"Kwa hivyo ili kuendeleza usitishaji huu wa uhasama, ni juu yao na huo ndiyo ujumbe wetu kwao: Kwamba hawawezi kushirikiana na makundi ya ndani ambayo siyo sehemu ya mapatano haya," alisema Toner katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washingotn.
Urusi na Marekani ndiyo walikuwa wafadhili wa pamoja wa mapatano ya usitishaji mapigano ya Fabruari 27, ambayo yalikuwa yameanza kusambaratika, hasa katika mkoa wa Aleppo. Mji huo umegawika kati ya vikosi vya Bashar al-Assad, vikosi vya magaidi vinyoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na kundi hatari la magaidi wa kundi la Jabhatu al-Nusra ambao si sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wiki iliyopita Urusi ilikubaliana na usitishaji mapigano katika mkoa wa Latakia na kiunga cha mji wa Damascus, lakini ikasema Assad anapaswa kuruhusiwa kupambana na magaidi wa Jabhatu al-Nusra mjini Aleppo ambao Marekani inawaita kuwa ni magaidi wa msimamo wa kati wasio na hatari. Mapigano makali yaliendelea mjini humo, na hospitali katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali na magaidi zilishambuliwa, mashambulizi ambayo wanadiplomasia wawili wa Umoja wa Mataifa walionya siku ya Jumatano kwamba ni uhalifu wa kivita.
Wahusika wawajibishwe
Afisa wa juu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman, na mkuu wake wa shughuli za misaada Stephen O'Brian, waliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba wanaohusika na mashambulizi dhidi ya hospitali na mizingiro ya kuwatesa watu katika maeneo yanayoshikiwa na waasi mjini Aleppo wanapaswa kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita.
Vita vya Syria vinavyochochewa na Marekani na washirika wake vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 270,000 mpaka sasa na mamilioni wameyakimbia makazi yao.
Hayo uanajiri huku serikali ya kifalme ya Saudia arabia ambayo haifuati misingi ya kidemokrasia ikiahidi kuendeleza kusaidia magaidi mpaka serikali ya Syria itoke madarakani.
Ufaransa ilitangaza jana kuwa itaitisha mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wanchi zinazounga mkono magaidi nchini Syria ikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu, Jumatatu ijayo, kujadili namna ya kusukuma mbele majadiliano yaliokwama.
Mwisho wa habari/ 291