Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Maafisa wa masuala ya uchaguzi nchini Venezuela wanatarajiwa kukutana leo hii kutowa uamuzi juu ya jaribio la upinzani kuitisha kura ya maoni kumuondowa madarakani Rais Nicolas Maduro kutokana na kusambaratika kwa uchumi wa nchi hiyo. Ushahidi unaonyesha kuwa serikali ya Marekani inatumia nguvu zake zote kushawishi machafuko katika nchi hiyo iliyopinga kabisa kutawaliwa na Marekani.
Baraza la Uchaguzi la Taifa (CNF) limeuwacha upinzani katika hali ya mashaka Jumanne iliopita ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho kutowa uamuzi wake iwapo wapinzani wa Maduro ambao wanaungwa mkono na Marekani wamefaulu kukusanya saini 200,000 kuwezesha kuitisha kura ya maoni dhidi ya kiongozi huyo wa sera za mrengo wa kushoto. Upinzani unahitaji kibali kutoka baraza hilo la uchaguzi kusonga mbele na mchakato huo wa kumn'gowa mdarakani rais ambaye wanamlaumu kwa uhaba wa chakula na mfumuko wa bei kupindukia pamoja na machafuko yanayozidi kuongezeka nchini humo. Badala ya kutowa uamuzi wao hapo Jumanne baraza hilo limesema halitokubali shinikizo na kuuahirisha uamuzi huo hadi Jumatatu kutafakari repoti ya wakaguzi wao juu ya ombi hilo la madai ya upinzani. Haijulikani wakati gani watatowa uamuzi wao huo.
Mwisho wa habari/ 291