Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: limemnukuu Saeed Khatibzadeh akisema hayo leo Ijumaa na mbali na kuipongeza serikali na wananchi wa Iraq katika sherehe na maadhimisho yao ya mwaka wa tatu tangu kulisambaratisha genge la kigaidi la Daesh na kuongeza kuwa, ushindi huo ni matunda ya nia ya kweli na jihadi imara iliyotokana na mshikamano baina ya serikali, wananchi na vikosi vyote vya ulinzi vya Iraq kwa msukumo wa kiongozi mkubwa wa kidini wa nchi hiyo, Ayatullah Sistani.
Aidha ameelezea jinsi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyowaunga mkono wananchi wa Iraq na serikali yao katika vita dhidi ya ugaidi hadi kulisambaratisha genge la kigaidi na ukufurishaji la ISIS na kuongeza kuwa, serikali na taifa la Iran muda wote liko pamoja na serikali na taifa la Iraq na halitoacha kulisaidia taifa hilo kwa msaada wowote litakaouhitajia kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wake, amani, utulivu, usalama na maendeleo yake.
Amesema, sote tumeona jinsi damu za mashahidi wa nchi hizi mbili za Iran na Iraq zilivyomwagika kwa pamoja katika vita hivi vitakatifu. Vile vile sote tumeona udugu na ushirikiano mkubwa uliojitokeza baina ya serikali za nchi hizi mbili baada ya kuuliwa shahidi, Luteni Jenerali Alhajj Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na shahid Abou Mahdi al Muhandis ambao ni makamanda wakubwa wa Iran na Iraq katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.
342/