Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wizara ya Afya ya Ujerumani ilitangaza habari hiyo jana Alkhamisi na kuongeza kuwa, mgonjwa huyo ni mwanamke ambaye aliwasili nchini Ujerumani tarehe 20 mwezi huu wa Disemba akitokea nchini Uingereza.
Nchi nyingi duniani hasa za Ulaya kama zimefunga mipaka yao na UIngereza baada ya kugunduliwa spishi mpya ya kirusi cha corona, kusini mwa nchi hiyo wiki iliyopita.
Jumatatu wiki hii, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alitangaza kuwa spishi mpya ya kirusi cha corona iliyogunduliwa nchini Uingereza inaambukiza na kuenea kwa kasi kubwa zaidi.
Dakta Tedros Adhanom Mkurugenzi wa WHO alieleza kuwa: spishi mpya ya kirusi cha corona iliyogundulwia huko Uingereza inaambukiza na kuenea kwa kasi zaidi hata hivyo hakuna ushahidi wa kuthitibisha kwamba kinauwa zaidi.
Maafisa wa Shirika la Afya Duniani Jumatatu wiki hii waliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kutoa ufafanuzi kuhusu spishi hiyo mpya ya kirusi cha corona ambayo kwa mara ya kwanza imegunduliwa nchini Uingereza.
Serikali ya waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, inashutumiwa na vyombo vya habari na fikra za walio wengi kutokana na kushindwa kukabiliana inavyopasa na maambukizo ya kirusi cha corona na hivyo imesababisha idadi kubwa ya wananchi wa Uingereza kuambukizwa na kupoteza maisha kwa ugonjwa huo hatari ulioenea dunia nzima.
342/