Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ali Larijani, Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran, katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Baghdad alisema: “Nadhani Hezbollah na harakati za muqawama wana kiwango kizuri sana cha ukuaji wa fikra za kisiasa na wanajua vizuri maslahi ya nchi zao, hivyo hawahitaji mlezi.”
Larijani aliendelea kusema: “Iran pia si nchi inayoweza kutikisika kwa upepo fulani kama baadhi ya watu wanavyofikiria.”
Akizungumzia kuhusu makubaliano ya kiusalama na Iraq, alisema kuwa mhimili mkuu wa makubaliano hayo ni kuhakikisha hakuna mtu au nchi yoyote itakayovuruga usalama wa mojawapo ya nchi hizi mbili, Iran na Iraq. Aliongeza kuwa lengo kuu la makubaliano hayo ni kuimarisha uthabiti wa uhusiano kati ya mataifa haya mawili.
Katibu huyo wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran alibainisha: “Tunaamini makubaliano haya ni mfumo wa ushirikiano wa kiusalama unaoweza pia kusambazwa kwa nchi nyingine, yaani wazo letu ni kwamba mataifa yote ya eneo hili yawe na usalama na nguvu.”
Larijani alisema: “Tunaamini makubaliano haya yanaweza kuenea hadi kwa mataifa mengine, kwa maana tuna mtazamo wa kuona kuwa mataifa yote ya eneo letu yawe salama na yenye nguvu.” Alisisitiza pia kuwa watu wa Iraq ni mashujaa na hawahitaji mtu wa kuwapa amri au kuwaelekeza.
Kauli ya Larijani inahusu makubaliano ya kiusalama kati ya Iran na Iraq yaliyosainiwa siku ya Jumatatu na yeye pamoja na Qasim al-Araji, mwenzake wa Iraq, mjini Baghdad.
Katika ziara yake mjini Baghdad, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran alikutana na Waziri Mkuu, Rais, Spika wa Bunge, Mshauri wa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa vya Iraq.
Your Comment