1 Septemba 2025 - 08:49
Source: Parstoday
Mkuu wa Jeshi la Lebanon apinga kupokonywa silaha wapiganaji wa Hizbullah

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Lebanon ametishia kujiuzulu kutokana na mpango wa kuipokonya silaha harakati ya Hizbullah.

Ni baada ya jeshi la Lebanon kupewa jukumu la kuandaa mpango wa kuipokonya silaha Hizbullah kufikia Jumapili hii, na kuutekeleza ifikapo mwisho wa mwaka, gazeti la The National News liliripoti jana Ijumaa.

Mkuu wa jeshi Lebanon, Brig Gen Rodolphe Haykal amesema hataki taasisi yake ikabiliane na Hizbullah moja kwa moja, akisisitiza kuwa ni suala lisilo sahihi kubuni mpango huo bila ushirikiano kutoka kwa harakati hiyo.

Afisa mmoja wa Lebanon amesema: "Brig Gen Rodolphe Haykal anataka serikali kufikia makubaliano ya kina na kuepuka kuliweka jeshi katika makabiliano ya moja kwa moja na Hizbullah na makundi mengine nchini Lebanon."

Gazeti la Al-Akhbar liliripoti jana Ijumaa kwamba baada ya kukutana na ujumbe wa Marekani na kusikia mashinikizo yao, Kamanda wa Jeshi la Lebanon, Jenerali Rodolphe Haykal, aliwaambia jamaa zake wa karibu kwamba atajiuzulu iwapo jeshi litalazimishwa kutekeleza mpango wa kuwapokonya silaha wapiganaji wa Hizbullah, na vikosi vya jeshi kuhusika katika umwagaji wa damu za Walebanon.

Harakati ya Hizbullah inasisitiza kuwa Israel lazima kwanza iondoke katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya kusini mwa Lebanon na kusitisha mashambulizi yake kabla ya kuanza mjadala wowote wa kuweka chini silaha. 

Your Comment

You are replying to: .
captcha