Bi Thunberg amesisitiza katika mahojiano aliyofanyiwa na Novara Media kwamba uanaharakati wake wa masuala ya hali ya hewa hauzuii kipaumbele anachotoa kwa Gaza na kwa Palestina.
Amesema, ikiwa unajali sayari ambapo binadamu wanaweza kuishi unapasa pia kuwajali binadamu. "Mimi si mwanaharakati wa masuala ya hali ya hewa kwa sababu tu nataka kuhudumia miti au chura," amesema Greta Thunberg.
Ameeleza kuwa utetezi wake wa haki za Wapalestina unatokana na yeye kuwa binadamu, "kuwa na hisia hai" na "maadili ya msingi."
Kesho Jumapili mwanaharakati huyo wa masuala ya hali ya hewa wa Sweden, Greta Thunberg atasafiri kwa meli hadi Gaza akitokea Barcelona katika msafara wa Global Sumud Flotilla, ambapo wataungana na maelfu ya wanaharakati katika misheni kubwa zaidi ya baharini kuwahi kuratibiwa kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
Thunberg amesema kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya mwamko wa kimataifa wa watu kutoka maeneo mbalimbali duniani wanaojaribu kuvunja mzingiro wa kikatili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment