1 Septemba 2025 - 08:51
Source: ABNA
Je, Ulaya imetumia kadi yake ya mwisho dhidi ya Iran?

Jarida la Foreign Policy limeashiria katika makala yake kuhusu hatua ya Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran (snapback) kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Jarida la Foreign Policy la Marekani limeeleza shaka kuhusu kufanikiwa utaratibu wa "Snapback" na kuandika kuwa: Kurejeshwa kwa vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran ni hatua ya kimaonyesho tu na hakuwezi kuathiri uchumi wa Iran, kama ilivyokuwa kwa vikwazo vya Marekani. Limeongeza kuwa: Hata kama Russia na China haziwezi kuzuia kurejeshwa vikwazo hivyo lakini nchi hizo zinaweza kuvuruga utekelezaji wake.  

Wiki iliyopita Iran ilipinga masharti yaliyotolewa na Ulaya kwa ajili ya kusitisha mchakato wa kurejeshwa vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu (snapback). 

Kwa mujibu wa masharti hayo, Iran lipasa kuwaruhusu wakaguziwa Wakala wa KImataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) bila kizuizi chochote, kuweka wazi mahali zilipohifadhiwa kilo 400 za mada ya urani iliyorutubishwa na kuanzisha tena mazungumzo na Marekani mkabala wa kusimamishwa kwa muda wa miezi sita urejeshwaji wa vikwazo dhidi yake. 

Foreign Policy imeandika kuwa" Hata hivyo mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yamepunguza hamu ya nchi hiyo kufanya mazungumzo au kuwaruhusu wakaguzi wa IAEA kufika katika taasisi zake za nyuklia.

Pamoja na haya, nchi tatu za Ulaya yaani Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilitaraji kuwa, kwa kutumia kadi ya mashinikizo ya mwisho na kuhuisha utekelezaji wa utaratibu wa Snapback zingeweza kubadili msimamo wa Iran, jambo ambao bila shaka inaonekana halitafanikiwai. 

Juzi Alhamisi, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zilianzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, unaojulikana kama "Snapback." Nchi hizo tatu za Ulaya, zinazojulikana kama E3, zote zilihusika katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015, ambayo yalilenga kuiondolea Iran vikwazo mkabala wa kupunguza uendelezaji wa miradi ya nyuklia ya Iran; hata hivyo Rais Donald Trump wa Marekani mwaka 2018 alitangaza kuiondoa nchi hiyo katika makubaliano hayo. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha