3 Septemba 2025 - 00:17
Source: Parstoday
Mkurugenzi wa klabu ya michezo ya Gaza auawa katika shambulilo la Israel akisubiri misaada

Shambulizi la anga la Israel ambalo lililenga umati wa watu waliokuwa wakisubiri misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Gaza limemuua pia Louay Estita, Mkurugenzi wa Klabu ya Michezo ya Gaza.

Louay Estita aliyekuwa na miaka 46 alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Gaza tangu mwaka 20215 na alikuwa mchezaji mashuhuri wa zamani wa mpira wa mikono. 

Israel usiku wa kuamkia juzi ilitekeleza shambulio la anga karibu na kivuko cha Zakim ambako mamia ya raia wa Palestina walikuwa wamekusanyika kupokea misaada ya kibinadamu. Klabu ya Michezo ya Gaza imetoa taarifa ikithibitisha kuuawa shahidi Estita na kubainisha masikitiko yake kuhusu kumpoteza mmoja wa shakhsia wake muhimu. 

Israel inaendelea kuwashambulia raia wa Palestina na miundombinu yake huku sekta ya michezo ya Palestina ikiwa imepata hasara na madhara makubwa. Jamii ya michezo ya wanamichezo wa Palestina imekuwa ikiyumba kutokana na athari za vita namauaji ya kibari ya Israel vinavyoendelea.

Jibril Rajoub Rais wa Chama cha Soka cha Palestina, hivi karibuni aliielezea hali hiyo kama "janga lisilo na mfano."

Tangu Oktoba 2023, takriban wanariadha 810 wa Palestina na maafisa wa michezo wameuawa katika mashambulizi ya Israel, wakiwemo wachezaji 423 wa kandanda, wanachama 387 wa mashirikisho mbalimbali ya michezo, na maskauti 142. Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na JIbril Rajoub kufikia mwezi huu wa Agosti .

Your Comment

You are replying to: .
captcha