Esmail Baqaei leo Jumanne ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa X kwamba: " "Tunaanza siku ya kwanza ya Mehr (mwezi wa kalenda ya Iran ya hijria shamsia) mwaka huu kwa kuwakumbuka na kuwanzi wanafunzi 34 waliouawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu."
Ameongeza kuwa: "Watoto wasio na hatia waliouawa wanakumbukwa pakubwa katika madarasa yao."
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewatakia wanafunzi wote hasa wale wa darasa la kwanza na walimu mwaka mwema wa masomo wenye mafanikio na kusisitiza kuwa wanafunzi na tumaini na tegemeo la nchi kwa ajili ya mustakbari bora.
tarehe 13 Juni mwaka huu Israel ilianzisha uvamizi wa wazi na usio na msingi dhidi ya Iran, na kusababisha vita vya siku 12 vilivyosababisha vifo vya takriban watu 1,064 nchini wakiwemo makamanda wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia na raia wa kawaida.
Marekani pia ilijiunga na uvamizi wa Israel kwa kutekeleza mashambulizi katika vituo vya nyuklia vya Iran hatua iliyotajwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Vikosi vya ulinzi vya Iranpia vilitoa mjibizo kwa kuvishambulia vituo na maeneo ya kimkakati ya Israel ikiwemo kambi ya al Udeid huko Qatar; kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.
Your Comment