Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, likinukuu Al-Mayadeen, «Abdullah Safi al-Din», mwakilishi wa Hezbollah ya Lebanon nchini Iran, alikutana na «Ali Akbar Velayati», Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu Masuala ya Kimataifa, na pande hizo mbili zilijadiliana maendeleo ya kikanda na kimataifa.
Ali Akbar Velayati, katika mkutano wake na Abdullah Safi al-Din, alisisitiza: “Iran, chini ya uongozi na maagizo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, itaendelea kwa uthabiti kuunga mkono Hezbollah, ambayo imesimama katika mstari wa mbele wa mapambano kama chombo cha thamani na kinachojitolea.”
Velayati aliongeza: "Hezbollah ni moja ya nguzo muhimu zaidi za Mbele ya Mapambano na inachukua jukumu la msingi katika kukabiliana na Uzayuni."
Safi al-Din pia alisema katika mkutano huo: "Hezbollah leo ina nguvu zaidi kuliko wakati wowote na iko tayari kutetea umoja wa ardhi ya Lebanon na watu wake, na haitaweka silaha zake chini kwa hali yoyote ile."
Akizungumzia ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita na utawala wa Kizayuni, alibainisha: "Utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wanapaswa kujua kwamba Hezbollah itajibu uvamizi kwa uthabiti wakati wowote inapoamua kufanya hivyo."
Mwakilishi huyo wa Hezbollah pia alishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hasa Kiongozi Muadhamu, kwa msaada wake kamili kwa mapambano ya Lebanon, na kusisitiza kwamba msaada huo ulisababisha utawala wa Kizayuni kwa mara ya kwanza kujitolea kufuata usitishaji vita ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa, jambo ambalo hatimaye lilipelekea kuwekwa imara kwa mipaka ya kusini ya Lebanon na Palestina inayokaliwa.
Your Comment