Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al-Mayadeen, Hani bin Brik, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Kusini (STC) linaloungwa mkono na Imarati amesema: "Saudi Arabia imeshambulia rasmi Hadramout na bandari yake ya kiraia kwa kisingizio cha uongo."
Kauli hizi za Bin Brik zimekuja kufuatia shambulio la leo asubuhi la muungano wa Saudia dhidi ya bandari ya Al-Mukalla katika mkoa wa Hadramout, ambapo mamluki wa Imarati wamewekwa.
Rashad al-Alimi, Mwenyekiti wa Baraza la Urais linaloungwa mkono na Saudi Arabia, pia alisisitiza: "Jukumu la Imarati ni dhidi ya watu wa Yemen na kuunga mkono waasi. Tunatangaza kufutwa kwa mkataba wa ulinzi wa pamoja na Imarati. Vikosi vya Imarati lazima viondoke Yemen ndani ya saa 24. Ninatangaza hali ya hatari nchini kote kwa siku 90."
Your Comment