Amir Saeid Iravani, katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kuhusu shambulio la Marekani dhidi ya Venezuela, alilaani vikali hatua hiyo na kuiita ugaidi wa kiserikali. Alisisitiza kuwa vitisho vya Trump dhidi ya Iran ni ukiukaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa. Aliongeza kuwa Marekani inawajibika kwa madhara ya uingiliaji wake, ikiwemo ushiriki wake katika mashambulizi ya Juni 2025.
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisema: "Marekani inadai kuwaunga mkono watu wa Iran, wakati huo huo ina historia ya wazi ya kuingilia kati na kuchukua hatua za kulazimisha za upande mmoja dhidi ya nchi hiyo."
Your Comment