6 Januari 2026 - 12:06
Source: ABNA
Sababu ya Trump kuwatupa kando wapinzani wa Venezuela kwa mujibu wa Wall Street Journal

Gazeti la Marekani limeripoti sababu ya Trump kupuuza uungaji mkono wa vuguvugu la upinzani nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa ABNA kupitia Al-Mayadeen, gazeti la Wall Street Journal liliripoti kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alipitia ripoti ya kijasusi inayoonyesha kuwa wapinzani wa Venezuela watakabiliwa na matatizo makubwa katika kuiongoza nchi kwa muda. Ripoti hiyo inasema watu bora zaidi wa kuiongoza Venezuela katika kipindi cha mpito baada ya Maduro ni shakhsia wanaonasibishwa na mfumo wa sasa wa nchi hiyo. Uchambuzi huu ni moja ya sababu zilizomfanya Trump kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Maduro badala ya kiongozi wa upinzani Maria Machado.

Your Comment

You are replying to: .
captcha