Kwa mujibu wa mwandishi wa ABNA akitoa taarifa kutoka kwa RT, katika ripoti rasmi iliyochapishwa na ofisi ya mkaguzi wa baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni imeelezwa kuwa uwezo wa utawala huu katika uzalishaji wa silaha pamoja na hifadhi zake za silaha umepungua kutokana na vita vya mfululizo tangu Oktoba 7.
Kulingana na ripoti hii, utegemezi unaoongezeka kwa uagizaji wa silaha kutoka nje unazuia upatikanaji wa jeshi wa hifadhi zinazohitajika katika uwanja wa vita. Licha ya uwekezaji wa mabilioni katika miundombinu ya uzalishaji wa silaha, uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya kijeshi katika utawala wa Kizayuni umeathirika.
Katika ripoti hii imeelezwa, baadhi ya mistari ya uzalishaji imepoteza uwezo wake kwa ukamilifu na mingine imedhoofika kwa sababu ya tabia ya Tel Aviv ya kununua malighafi nafuu kutoka nje na kutokukidhi mahitaji ya viwanda vya ndani.
Kulingana na ripoti hii, kujenga upya uwezo wa uzalishaji wa vitengo hivi kunahitaji uwekezaji mkubwa na muda mrefu, jambo ambalo limeifanya utawala wa Kizayuni uwe katika hali dhaifu kwa sababu ya vita vya mfululizo. Ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kivita umesababisha kupungua kwa operesheni katika nyuga mbalimbali. Vita vilivyopiganwa vilifichua moja ya udhaifu wa kina kabisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni; kizuizi cha kuingia katika vita vya muda mrefu bila msaada wa moja kwa moja wa nje katika kupokea silaha na risasi. Migogoro ya muda mrefu na vikosi vya upinzani huko Gaza, Hizbullah, Iran na Yemen imetumia sehemu kubwa ya hifadhi za kijeshi za utawala wa Kizayuni.
Your Comment