20 Juni 2026 - 19:40
Mchambuzi: “Heiba ya Marekani Yaporomoka Mbele ya Muqawama; Ushindi Wake Ni kwa Serikali Tegemezi Pekee”

Dkt. Hassan al-Rassabi: “Marekani haijashinda dhidi ya mataifa ya Muqawama, bali imefanikiwa tu kwa serikali tegemezi; heba ya Washington imeporomoka kimkakati.”

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Dkt. Hassan Hussein al-Rassabi ameandika uchambuzi mkali kuhusu kile alichokiita “kuporomoka kwa haiba ya Marekani” mbele ya Mhimili wa Mapambano ya Muqawama (Axis of Resistance), akisema kauli za ushindi wa Washington ni za uongo na propaganda za kisiasa.

Al-Rassabi amesema kuwa wakati baadhi ya vyombo vya habari na vyanzo vya Magharibi vinadai Marekani imepata ushindi, hali halisi inaonyesha kuwa taasisi za kijeshi za Marekani zimekiri kushindwa kwao kimkakati katika eneo la Mashariki ya Kati.

Ameongeza kuwa Marekani haijashinda dhidi ya Iran, Yemen, Gaza wala Lebanon, bali imefanikiwa tu kwa baadhi ya serikali tegemezi ambazo, kwa mujibu wake, zimekuwa zikitumia rasilimali zao kwa ununuzi wa silaha na kuingia katika mifumo ya kiusalama inayodhibitiwa na Washington.

Aidha, ameonya kuwa mwenendo huo wa utegemezi wa kisiasa na kiusalama unaweza kuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa mataifa hayo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha