Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa sharti la kufanyika kwa mazungumzo ya dhati na yenye matokeo ni kuwa na utayari kamili wa kukabiliana na vita.
Qalibaf alitoa kauli hiyo alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais wa Yemen, ambapo alieleza kuwa Marekani pamoja na utawala wa
Kizayuni wamelazimika kutambua nafasi na ushawishi wa washirika wa Iran ndani ya mhimili wa muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati.
Alisisitiza kuwa nguvu ya muqawama imebadili mizani ya kisiasa na kijeshi katika eneo hilo, na kwamba mazungumzo yoyote ya maana yanahitaji msingi wa nguvu na utayari wa kujilinda, badala ya udhaifu.
Qalibaf aliongeza kuwa Iran itaendelea kuwaunga mkono washirika wake katika mhimili wa muqawama na haitakubali shinikizo au vitisho vinavyolenga kudhoofisha usalama na maslahi ya mataifa ya eneo hilo.
Your Comment