6 Julai 2026 - 23:06
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatamul Al-Anbiya Ampongeza Mohseni-Ejei kwa Kuteuliwa Tena Kuongoza Mhimili wa Mahakama

Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (s), Meja Jenerali Ali Abdollahi, amesema kutekeleza maelekezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuzingatia matarajio ya Kiongozi Shahidi kutahakikisha mafanikio endelevu ya Mkuu wa Mhimili wa Mahakama wa Iran.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s), Ali Abdollahi, amemtumia ujumbe wa pongezi Gholam-Hossein Mohseni-Ejei kufuatia kuteuliwa tena kuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama wa Iran.

Katika ujumbe huo, Abdollahi alisema kuwa uteuzi huo unaonyesha imani na uongozi wenye hekima wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na kutambua uwezo, uadilifu na uzoefu wa Mohseni-Ejei katika kuongoza mfumo wa mahakama nchini.

Alisisitiza kuwa kuweka mbele matarajio yaliyobainishwa na Kiongozi wa Mapinduzi katika ujumbe wake wa hivi karibuni, pamoja na kuendeleza maono ya Kiongozi Shahidi, hasa katika utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya mfumo wa mahakama na kutumia uzoefu wa viongozi waliotangulia, kutakuwa msingi wa mafanikio zaidi katika nafasi hiyo nyeti.

Aidha, Kamanda huyo alitangaza utayari wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya na vikosi vya ulinzi vya Iran kushirikiana na Mhimili wa Mahakama ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake, huku akimuombea Mohseni-Ejei na watumishi wote wa mahakama mafanikio katika kuwahudumia wananchi na kusimamia haki.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha