13 Julai 2026 - 23:37
IRGC Yatangaza Kushambulia Miundombinu ya Kijeshi ya Marekani nchini Bahrain na Mifumo ya Rada Nchini Oman

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa limeharibu miundombinu ya kijeshi ya Marekani nchini Bahrain pamoja na mifumo ya rada nchini Oman, likisema operesheni hiyo ni sehemu ya awamu ya tano ya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa katika awamu ya tano ya operesheni zake za kulipiza kisasi, vikosi vya wanamaji vya jeshi hilo vimefanya mashambulizi dhidi ya miundombinu na vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo katika eneo la Juffair nchini Bahrain.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na IRGC, mashambulizi hayo yalihusisha matumizi ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones), ambapo pia yalidai kulenga na kuharibu rada ya masafa marefu ya anga aina ya **FPS**, pamoja na rada ya kugundua vyombo vya majini iliyoko nchini Oman.
 
IRGC imesema operesheni hiyo inalenga kujibu kile ilichokitaja kuwa uingiliaji wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kwamba mashambulizi hayo ni sehemu ya mkakati wake wa kulinda usalama wa taifa na maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 
Katika taarifa hiyo, IRGC imesisitiza kuwa njia pekee ya kurejesha usalama wa usafiri wa meli katika Mlango wa Bahari wa Hormuz ni Marekani kusitisha uingiliaji wake wa kijeshi na kuheshimu mamlaka ya mataifa ya eneo hilo juu ya maji yao ya pwani.
 
Aidha, jeshi hilo limeonya kuwa kuendelea kwa hali hiyo kunaweza kusababisha athari kubwa zaidi kwa usafirishaji wa mafuta na gesi duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha