Akizungumza katika mkutano wake wa pamoja na waandishi wa habari na mgeni wake Ali Akbar Saleh Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Waziri huo wa Uturuki amesema bayana kwamba, nchi yake haiamini hata kidogo kama Iran ilihusika katika njama hiyo. Ameongeza kuwa, kwa mtazamo wa Uturuki madai hayo ya Marekani dhidi ya Iran hayana msingi wowote. Kwa upande wake Ali Akbar Saleh amesema, madai hayo ni mlolongo wa propaganda zisizo na msingi za Marekani dhidi ya Iran na kubainisha kwamba, iko siku viongozi wa Marekani watalazimika kuiomba radhi Tehran kwa tuhuma hii. Itakumbwa kuwa, hivi karibuni Marekani iliituhumu Iran kwamba, eti ilihusika katika njama iliyofeli ya kutaka kumuua balozi wa Saudia nchini Marekani, madai ambayo yametajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni ya kipuuzi na kitoto.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273608
Abna inatuarifu kuwa:Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki amesema, madai ya serikali ya Marekani dhidi ya Iran hayana msingi wowote ule. Ahmet Davotuglu amesema, Marekani imeshindwa kuthibitisha madai yake kwamba Iran ilihusika katika njama iliyofeli ya kutaka kumuua balozi wa Saudia nchini Marekani.