Abna inatuarifu kuwa:Timu za uokozi zinaendelea na kazi ya kuwatafuta watu wanaosadikiwa kufunikwa na vifusi baada ya mtetemeko huo wa ardhi uliotokea usiku wa kuamkia jana mashariki mwa Uturuki. Duru rasmi za Uturuki zimetangaza kwamba, hadi sasa watu 272 wamethibitishwa kupoteza maisha yao katika baa hilo; ingawa kuna wasi wasi wa kuongezeka kwa idadi hiyo kutokana na watu wengi kudhaniwa kuwa wamefunikwa na vifusi baada ya majengo mengi kubomolewa na mtetemeko huo wa ardhi. Idris Naim, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametangaza kwamba, watu 95 wamethibitishwa kupoteza maisha yao katika mji wa Van na 169 katika Wilaya ya Ercis. Tetemeko baya kabisa la ardhi kuwahi kuikumba Uturuki lilikuwa lile la mwaka 1999 ambapo watu wapatao 20,000 walipoteza maisha yao kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 274263
Idadi ya watu waliopoteza maisha katika janga la kimaumbile la mtetemeko wa ardhi nchini Uturuki imeongeza na kukaribia 300.