19 Machi 2011 - 20:30

Abna inatuarifu kuwa:Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mgogoro wa chakula nchini Niger karibuni hivi, baada ya mazao kuliwa na wadudu.

Denis Brown, Mkuu wa Kuratibu Mpango wa Chakula Duniani nchini Niger amesema kuwa ukosefu mkubwa wa nafaka unaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa chakula kama ule ulioshuhudiwa nchini humo mwaka 2005 na 2010. Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umetangaza kwamba, familia zilizokubwa na njaa mwaka uliopita bado zinakabiliwa na tatizo hilo. Katika upande mwingine WFP imesema kwamba inaongeza kiwango cha operesheni zake nchini Niger ambapo dola milioni 60 zinatakiwa kufadhili misaada ya chakua kwa kipindi cha miezi 6 ijayo.Taarifa hiyo imesema kuwa, ukame wa muda mrefu unazidi kushuhudiwa katika maeneo ya pwani ya Niger. WFP imetangaza pia kuwa ukame umetokea pia katika nchi za Chad, Burkina Faso na Mauritania.