Waziri Mkuu mpya wa Madagascar amechaguliwa katika fremu ya utekelezaji wa mpango wa ramani ya njia wenye lengo la kuiondoa Madagascar katika mgogoro na kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na pande zote husika za kisiasa nchini humo. Rajoelina amesema amemteuwa Beriziky kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya mpito kutokana na kiongozi huyo kuwa mzalendo, kumjua Mwenyezi Mungu na uwezo wake katika kuongoza taasisi mbalimbali na na kufanya mazungumzo na pande za kimataifa. Omer Beriziky ana rekodi nzuri ya uongozi kwani aliwahi kuwa balozi wa Madagascar nchini Ubelgiji, mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya na Mkuu wa Kamati ya Mabalozi wa Kiafrika, Caribbean na Oceania. Beriziky amechukua nafasi ya Albert Camille Vital Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu wadhifa huo tarehe 17 mwezi huu. Beriziky ana siku 15 za kutangaza baraza jipya la mawaziri huko Madagascar. Weledi wa mambo wanataraji kuwa kuteuliwa Waziri Mkuu huyo Mpya na kusainiwa ramani ya njia ya Madagascar ni hatua nzuri itakayoisaidia Madagascar kujiondoa katika hali ya mgogoro wa kisiasa uliyodumu kwa miaka kadhaa. Mpango wa ramani ya njia ya Madagascar uliosainiwa na pande zinazozozana nchini humo tarehe 17 mwezi Septemba mwaka huu, ni makubaliano ya tatu rasmi baada ya yale ya Maputo na Addis Ababa yaliyosainiwa mwaka 2000 ili kuisaidia Madagascar kujiondoa katika hali ya mgogoro. Ramani ya njia ya Madagascar ilisainiwa na makundi nane ya kisiasa mwezi Machi uliopita. Hata hivyo harakati ya marais wa zamani wa nchi hiyo yaani Marc Ravalomanana, Didier Ratsiraka na Albert Zaky, imepinga mpango huo. Suala la kurejea nchini Madagascar Ravalomanana ndilo lililokuwa likizusha hitilafu kati ya pande zinazozozana nchini humo. Viongozi wa SADC wametaka kurejea Ravalomanana kutoka uhamishoni bila ya masharti yoyote. Hii ni katika hali ambayo serikali ya mpito ya Madagascar ilipinga pendekezo hilo la SADC na kutangaza kuwa itamtia nguvuni na kumfunga jela Marc Ravalomanana atakaporejea nchini. Kutolewa amri ya kuuwa waandamanaji wa harakati ya wafuasi wa demokrasia huko Madagascar miaka miwili iliyopita ni miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Ravalomanana. Hata hivyo hatimaye Rajoelina ametupilia mbali msimamo wake mkali wa zamani na kukubali kuandaa uwanja wa kupasishwa ramani hiyo ya njia kwa kukubali kurejea nchini wakimbizi wa kisiasa na kusainiwa ramani hiyo ya njia mwezi Septemba mwaka huu.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 275248
Andre Rajoelina Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Ijumaa ya jana alimteuwa Omer Beriziky kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.