19 Machi 2011 - 20:30

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kukomesha mashambulio yake ya kinyama katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina.

Abna inatuarifu kuwa:Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kukomesha mashambulio yake ya kinyama katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina. Ban Ki-Moon ameelezea wasi wasi mkubwa wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuongezeka wimbi la mashambulio huko Gaza. Wakati huo huo Russia imesema kuwa, kushadidi kwa vitendo vya mauaji huko Palestina ni kwa maslahi ya watu wasiotaka kuona amani na usalama vinashuhudiwa katika Mashariki ya Kati. Juzi usiku ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zilifanya mashambulizi kusini mwa Ukanda wa Gaza na kupelekea kuuawa shahidi Wapalestina wasiopungua 10.