19 Machi 2011 - 20:30

Viongozi wa Baraza la Mpito la Taifa la Libya wametangaza leo kuwa rundo la silaha za kemikali zimepatikana nchini humo, huku leo ikiwa ni siku ambayo Jumuiya ya kijeshi ya NATO inakamilisha operesheni zake za kijeshi nchini humo.

Ripoti ya ABNA- Mahmoud Jibril kiongozi nambari mbili wa Libya amesema kwamba silaha hizo za kemikali zimepatikana katika miji miwili tofauti na kwamba ameitaarifu Jumuiya ya Kupiga Marufuku Silaha za Kemikali yenye makao yake huko The Hague itakayochukua hatua zinazotakiwa kulinda maeneo yenye silaha hizo. Wakati huo huo, Baraza la Taifa la Mpito la Libya limesema kwamba linaamini kuwa mamia ya sarafu za kale za nchi hiyo zilizoibiwa katika benki ya Benghazi wakati wa harakati za mapinduzi zimepelekwa nchini Misri. Zaidi ya sarafu 7,000 zenye thamani na vyombo vya kale viliibiwa mwezi Mei wakati wa mapigano dhidi ya vikosi vya Muammar Gaddafi katika mji huo.