Akizungumza na kanali ya televisheni ya CNN ya Marekani, Jibril amesema kuwa walitaraji kwamba Gaddafi asingeuliwa na badala yake angetiwa nguvuni. Hii ni kwa sababu Gaddafi alikuwa na siri nyingi ambapo kwa kuweko kwake wangeweza kufahamu waziwazi namna alivyokuwa na mahusiano na nchi na viongozi wengi duniani. Jibril ameongeza kuwa hakukuwa na sababu ya kuuawa kirahisi Muammar Gaddafi na kwamba iwapo wanamapinduzi wa Libya wangetaka kumuua, basi wangeweza kufanya hivyo tangu awali walipomkamata, hata hivyo si jambo la kawaida kuona Gaddafi aliuawa ghafla mara baada ya wanamapinduzi kumkamata na kumshikilia kwa muda. Amesema hilo lenyewe linaonyesha kuwa baadhi ya wanamapinduzi wa Libya walipewa amri ya kumuua Gaddafi na duru za kigeni zisizofahamika.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 277376
Mahmoud Jibril Mkuu wa utendaji wa zamani wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya amesema kuwa Muammar Gaddafi kiongozi wa zamani wa nchi hiyo aliuawa na pande za kigeni baada ya kutiwa mbaroni.