19 Machi 2011 - 20:30

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Luis Moreno Ocampo ametangaza kuwa mwana wa dikteta wa zamani wa Libya Saiful Islam Gaddafi atatiwa nguvuni muda si mrefu

Ocampo amesema swali linaloulizwa kwa sasa si kuhusu suala la kutiwa nguvuni Saiful Islam bali ni kuhusu lini atatiwa nguvuni.Ocampo amesema kuwa awali kulifanyika mazungumzo baina ya mahakama ya ICC na Saiful Islam kupitia jamaa zake wa karibu ingawa amesisitiza kuwa hajui mahapa alipo mwana huyo wa Gaddafi anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu.Wakati huo huo serikali ya Niger imetangaza kuwa watu 14 wameuwa katika mapigano makali yaliyotokea kwenye mpaka wake na Algeria baina ya jeshi la nchi hiyo na msafara uliokuwa ukiongozwa na wapiganaji wa Kitouareg. Baadhi ya askari wa Niger wanasisitiza kuwa msafara huo ulikuwa na Walibya watiifu kwa dikteta aliyeuawa wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.