19 Machi 2011 - 20:30

Wananchi wa Syria wamevamia ubalozi za Saudi Arabia na Qatar mjini Damascus kulaani hatua ya nchi hizo kuongoza hatua ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kusimamisha uanachama wa Syria, aidha waandamanaji wenye hasira Syria pia wameandamana nje ya ubalozi wa Marekani.

Wananchi wa Syria wanasema Marekani imezichochea nchi za Kiarabu dhidi ya Syria. Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imedai kuwa imelazimika kusimamisha uanachama wa Syria kutokana na kushindwa serikali ya Rais Bashar al Assad kusitisha machafuko nchini humo kufikia Novemba 2 kama ilivyotakiwa. Katika hali ambayo upinzani umekuwa ukivituhumu vyombo vya usalama Syria kuwa vinatumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji, serikali ya Damascus imekuwa ikisisitiza kuwa, magenge ya wabeba silaha yenye kuungwa mkono na nchi za kigeni ndiyo yanayochochea machafuko nchini humo