Watu 17 wamepoteza maisha yao kufuatia mlipuko katika ghala la silaha la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, magharibi mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.Mkuu wa uhusiano wa ummah katika IRGC Luteni Generali Ramezan Sharif (kwenye picha kushoto) amesema watu wengine 16 wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliojiri Jumamosi karibu saa saba kamili mchana kwa saa za Tehran. Imearifiwa kuwa mlipuko huo ulitokea pale silaha zilipokuwa zikibebwa kuelekezwa eneo la oparesheni. Uchunguzi kuhusu chanzo cha mlipuko huo umeanza.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 278077
Watu 17 wamepoteza maisha yao kufuatia mlipuko katika ghala la silaha la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, magharibi mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.