19 Machi 2011 - 20:30

Kwa akali askari 20 na raia 14 wameuawa kufuatia mashambulio ya maroketi yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la ash Shabaab la Somalia

Habari zinasema kuwa, wanamgambo hao wa ash Shabaab wamezishambulia kwa maroketi kambi za jeshi la serikali ya mpito ya Somalia katika wilaya ya Huriwa, kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu na kuua askari 20. Shambulio la pili la wanamgambo wa ash Shabaab lililotokea katika wilaya ya Dayniile limepelekea kuuawa raia wasiopungua 14. Habari zaidi zinasema kuwa, watu wanne wa familia moja ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la jana wilayani Dayniile. Kundi hilo la ash Shabaab lenye misimamo ya kufurutu ada linakabiliwa na mashambulizi makali ya jeshi la Kenya yaliyoanza katikati ya mwezi uliopita wa Oktoba. Somalia imekuwa haina serikali kuu yenye nguvu tokea mwaka 1991, baada ya kuangushwa utawala wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika Siad Barre.