Sergey Lavrov ametahadharisha pia kuwa, kuchochea machafuko nchini Syria ni hatari kwa usalama wa nchi zote za Kiarabu.Amesema msimamo wa kiadui wa nchi za Magharibi kuhusiana na Syria umechochea kushadidi maandamano dhidi ya serikali katika nchi za Misri, Bahrain na Kuwait.Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia ametaka waachiwe Wasyria wajiamulie wenyewe mambo yao bila kufanywa uchochezi wa aina yoyote ile.Aidha ameashiria uharibifu mkubwa uliofanywa na Magharibi nchini Libya kupitia jeshi la NATO na kuongeza kuwa, Russia haitaruhusu nchi za Magharibi zitumie tena vibaya sheria za kimataifa dhidi ya Syria.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 279708
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezishambulia vikali nchi za Magharibi kwa kuchochea machafuko nchini Syria.