Tume ya Uchaguzi ya Kongo imekuwa ikitangaza matokeo ya kura zinazohesabiwa kila siku. Imesema kuwa matokeo ya kura zilizohesabiwa hadi sasa yanaonyesha kuwa Joseph Kabila anaongoza akifuatiwa na mpinzani wake mkuu mwanasiasa mkongwe wa nchi hiyo mzee Etienne Tshisekedi. Wapinzani nchini Kongo wanalalamika kwa kuhoji kuwa kwa nini Tume ya Uchaguzi haitangazi kura hizo zilizohesabiwa hadi sasa ni za maeneo yepi ya uchaguzi. Wasiwasi umeongezeka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukiwa na hofu ya kujiri mapigano baada ya kila mmoja kati ya wagombea wawili wa kiti cha urais nchini humo yaani Joseph Kabila na Etienne Tshisekedi kujitangaza mshindi wa uchaguzi huo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 282396
Zoezi la kuhesbu kura za uchaguzi wa Rais na Bunge uliofanyika tarehe 28 mwezi Novemba mwaka huu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lingali linaendelea.