19 Machi 2011 - 20:30

Ujerumani imesema kuwa itaendelea kutoa mafunzo ya kijeshi kwa askari wa Misri, licha utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaofanya na askari hao dhidi ya waandamanaji katika Medani ya Tahrir mjini Cairo

Ujerumani imesema kuwa itaendelea kutoa mafunzo ya kijeshi kwa askari wa Misri, licha utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaofanya na askari hao dhidi ya waandamanaji katika Medani ya Tahrir mjini Cairo. Ikijibu barua ya mbunge wa upinzani wa Misri, Niema Movassat aliyetoa wito wa kusimamishwa utoaji wa mafunzo hayo ya kijeshi, Wizara ya Ulinzi wa Ujerumani imesema mpango huo wa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa askari wa Misri hautositishwa kwani una umuhimu mkubwa. Jeshi la Ujerumani huwapa mafunzo askari 10 wa Kimisri kila mwaka.Hii ni katika hali ambayo, Watu 10 wameliwa na askari wa Misri katika machafuko ya siku mbili kwenye Medani ya Tahrir mjini Cairo huku wengine 300 wakijeruhiwa. Waandamanaji nchini Misri wanataka baraza la kijeshi likabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia.