19 Machi 2011 - 20:30

ABNA inasikitika kutuarifu kuwa:Kim Jong-il Kiongozi wa Korea Kaskazini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69. Jong-il ambaye ameliongoza taifa hilo la kikomonisti tangu alipofariki dunia baba yake mwaka 1994, amefariki dunia akiwa katika treni wakati alipokuwa akitembelea eneo moja la nje ya mji mkuu wa nchi hiyo, Pyongyang.

Taarifa rasmi iliyotangazwa na nchi hiyo inasema kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini amefariki dunia kutokana na mshituko wa moyo. Kufuata kifo cha Kim Jong-il, Rais wa Korea Kusini ametangaza kwamba nchi hiyo iko katika hali ya tahadhari na ameitisha kikao cha wajumbe wa Baraza la Usalama la Taifa. Mwana wa kiume wa tatu wa kiongozi huyo Kim Jong-Un ametangazwa kuwa ndiye atakayemrithi baba yake. Mazishi ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini yatafanyika mjini Pyongyang tarehe 28 Disemba huku taifa la nchi hiyo likiomboleza hadi tarehe 29 mwezi huu. Marekani na madola mengine yenye uadui na nchi hiyo yametangaza kwamba yanafuatilia kwa karibu yanayojiri Pyongyang baada ya kifo cha Kim Jong-ili aliyewaumiza vichwa Wamagharibi kwa kuliwezesha taifa la Korea Kaskazini kumiliki silaha za nyuklia.