19 Machi 2011 - 20:30

Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeanza mazoezi ya siku kumi yaliyopoewa jina la "Velayat 90

Maneva hiyo iliyoanza Jumamosi itaenea katika eneo kubwa kutoka mashariki mwa Lango la Hormuz katika Ghuba ya Uajemi hadi eneo la Ghuba ya Aden.Katika mazoezi hayo yaliyoanza Jumamosi, Jeshi la Wanamaji la Iran litaonyesha zana zake mpya kabisa pamoja na ubunifu wake. Nyambizi kadhaa zikiwemo Tareq na Ghadir, manoari, mfumo wa makombora ya ardhi-kwa-bahari na torpedo ni kati ya zana zitakazoonyeshwa katika maneva hiyo. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji Iran Admeli Habibollah Sayyari amekanusha ripoti kuwa Lango la Hormuz litafungwa siku moja kwa ajili ya mazoezi hayo.Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta ya ulinzi na sasa inajitosheleza katika uzalishaji wa zana muhimu za kivita. Iran inasisitiza kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi unalenga kuihami nchi na wala si tishio kwa nchi zingine.