19 Machi 2011 - 20:30

Balozi wa Afrika Kusini katika Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya NATO wakati wa harakati za kuuangusha utawala wa dikteta Muammar Gaddafi wa Libya.

Baso Sangqu, ambaye hivi sasa ndiye rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema anaamini kuwa NATO ilikanyaga haki za binadamu wakati wa kutekeleza agizo la kutopaa ndege katika anga ya Libya wakati wa harakati za kumuondoa dikteta Gaddafi madarakani. Hata hivyo, Msemaji wa NATO Oana Longescu amekanusha madai hayo na kusema kuwa, vikosi hivyo vilifanya kila lililowezekana kupunguza maafa ya raia. Mwishoni mwa mwezi uliopita, Vitaly Churkin Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alitaka ufanyike uchunguzi wa kina kuhusu vifo vya raia vilivyotokea huko Libya wakati wa oparesheni za NATO nchini humo.