19 Machi 2011 - 20:30

Rais wa Siria amelihutubia taifa na kuitupia lawama jumuiya ya nchi za Kiarabu kwa kujaribu kuiyumbisha Syria.

Rais Bashar al Assad alisema " Hii jumuiya ya nchi za Kiarabu na ufalme wao wana  haki gani ya kutufundisha sisi wa Siria. Bunge la kwanza la Siria lilikuwa mwaka 1917, je hizi nchi za kifalme zilikuwa wapi? na  vurugu na mashambulizi yanayo tokea nchini Siria ni ya makundi ya kigaidi ambayo yanapata misaada toka nchi za nje. "Hali hii ni sawa na tabibu kumkataza mgonjwa asivute sigara, ilihali tabibu anasigara mdomoni." "Sijawahi kutoa ruhusa ya kuwa watu wapigwe risasi, na kutoka kwangu madarakani kutakuwa ni maamuzi ya wanachi."  Alisema rais Assad. Rais Bashar al-Assad alitoa hotuba hiyo kwenye chuo kikuu  Damascus.ni mwezi mmoja sasa tangu waangalizi 165 wa jumuiya ya nchi za Kiarabu waingie nchini Siria ili kukagua hali halisi ya vurugu zinazo endelea.