19 Machi 2011 - 20:30

Aliyekuwa rais wa Pakistan na ambaye anaishi nchi Uingereza, amechelewesha nia yake ya kurudi nyumbani Pakistan, baada ya kutishiwa kukamatwa iwapo ataweka nyanyo zake katika ardhi ya nchi hiyo..

Pevez Musharraf ambaye alikuwa rais wa Pakistan na mkuu wa jeshi, ambaye baada ya kuachia madaraka mnamo mwaka  2008 alihamia Uingereza na baadaye mapema miaka miwili alitangaza kurudi nyumbani kwa dhamira ya  kugombania kiti hicho cha urais kwa mara nyingine tena, kwa kupitia chama chake All Pakistan Muslim League.bwana:Muhammad Ali Saif  Msemaji wa chama cha All Pakistan Muslim League alisema:" Uamuzi wa kuahirisha safari ya  kurudi nyumbani kwa Pevez Musharraf ni uamuzi ambao chama kilimlazimisha kufanya hivyo baada ya kukaa kikao kwa muda wa masaa  mawili, jambo ambalo Pevez Musharraf alikuwa amelipinga."Na chama kitaamua lini Pevez Musharraf atarudi nyumbani Pakistan."Uamuzi wa  kuimzuia Pevez Musharaf asirudi Pakistan, umekuja baada ya bunge kupitisha uamuzi ya kuwa akirudi nyumbani lazima akamatwe.