Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Sheikh Hasan Farhan Al malikiy katika kuhami Wananchi wa Bahrain na kuwa kwao na Subira na maandamano ya amani katika Nchi hiyo aliwapongeza kwa kazi wanayofanya.
Pia akiwambia Viongozi wa Nchi za Kiarabu kunako uvamizi wa Kijeshi Nchi ya Syria na Yemen kueleza kua badala ya kuvamia Syria na Yemen tuwakumbuke wa Bahrain ili kuwatoa katika hali waliokuwemo sasa na lazima kuwapoza kwa matatizo walokuwa nayo.
Sheikh Hasan Farhan Al malikiy alisema:Mapinduzi ya Bahrain yanazingatia tamaduni na haki za Binadamu kwani mapinduzi na maandamano yao ni tofauti na ya Nchi zingine za Kiarabu kuhifadhi amani na ulivu wa Nchi.
Akiendelea kusema: Msimamo walokuwa nao Wananchi wa Bahrain kwa kufungiwa kila njia ya mawasiliano hiyo ni bishra njema ya ushindi wa mapinduzi ya Wananchi hao.
Sheikh Farhan Al malikiy alisisitiza kwa kile kinacho fanywa na utawala wa Alikhalifa kuakandamiza waandamanaji kuanyima hakizao bila kutosheka na hayo kuwateka nyara na kutia mbaroni waandamanaji na kuawa, kuadhibu, kushika Wanawake waoandamana, kushika madaktari wanaosaidia majeruhi ya waandamanaji, na wanamichezo waliounga mkono waanadanaji, na suala hili limewakera sana watetezi wa haki za Binadamu.
La kuzingatia ni kwamba Sheikh Farhan Malakiy ni miongoni mwa wahakiki wa Saudia Arabia na katunga Vitabu vingi.
Sheikh Hasan Farhan Al Malikiy kutokana na kutunga vitabu vya dhidi ya fikra za kiwahabi na kuzagaza vitabu vyake alitiwa mbaroni mara kadhaa.