11 Agosti 2012 - 19:30

Takribani zaidi ya watu 120 wamepoteza maisha na zaidi ya 1,500 wamejeruhiwa na matetemeko pacha ya ardhi ambayo yamepiga mkoa wa Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran jana Jumamosi.

Khalil Saie, mkuu wa Kituo cha majanga ya asili cha Azerbaijan Mashariki amesema katika televisheni ya taifa kwamba idadi inaweza kuwa kubwa kutokana na nguvu ya matetemeko.

Matetemeko hayo pacha yaliyopiga kwa dakika 11 kila moja yalikuwa na ukubwa wa kipimo cha 6.2 na 6.0 kwa mujibu wa chuo kikuu cha Tehran