Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atahudhuria siku ya Alhamisi na Ijumaa ya Wiki hii katika Mkutano wa 16 wa Jumuiya ya NAM Tehran 2012.
Kulingana na ripoti ya Mahdi Akhund Zadeh msaidizi wa Kimataifa wa Wizara ya mambo ya nje Iran; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwa muda atakao kuwa Iran atahudhuria katika Vino vya Nyuklia Natanz na Isfahan.
Ripoti kutoka katika Nchi 1+5 wamedai kuwa Nyuklia ya Iran si ya amani lengo lao ni silaha za maangamizi.
Baadhi ya Nchi za Magharibi ikiwemo Marekani yashadidisha kuwekewa vikwazo Iran na kuomba Umoja wa Kimataifa kupitisha hilo.