Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA: taasisi inayosimamia masuala ya hija nchini Nigeria imeainisha msimamo wake rasmi wakuto kwenda hija ya mwaka huu nchini Saudi Arabia, baada ya serikali ya Saudi Arabia kuwazuia wanawake elfu moja kuingia Saudia kwa kisingizio cha kusafiri pasina maharimu zao. Katika hali hiyo ya kuzuiwa wanawake hao kuingia Saudi Arabia, nchi ya Nigeria nayo imetangaza kuwa siruhusa kwa wananchi wake kushiriki katika Hija ya mwaka huu.Katika hali hiyo balozi wa Nigeria nchini Saudi Arabia baada ya kutangazwa habari ya kuzuliwa wanake hao amesema: mpaka sasa viongozi wa Nigeria katika kujibu mwendo mbaya wa Saudia Arabia na akina mama wa kinigeria wameamua kuwazuia wanigeria wote kuhiji mwaka huu, kwaminajili hiyo ndege zote zinazoelekea nchini Saudia kuanzia sasa zimesimamishwa mpaka itakapo tangazwa.
29 Septemba 2012 - 20:30
Msimbo wa Habari: 352394
Katika masiku ya mwisho ya wiki iliopita vyombo vya habari vya nchi za kiarabu vimetangaza kuwa Saudi Arabia amewaziwia wanawake elfu moja wakinigeria walikuwa wamekusudia kuhiji mwaka huu