5 Novemba 2012 - 09:46

Wizara ya Upelelezi ya Iraq imeeleza kuwa imefaanikiwa kumshika msababishi wa miripuko ya Kadhimain na Jakuk.

 Ripoti ya shirika la habari la Ahlu Bayt(as) -ABNA-  Wizara ya Upelelezi ya Iraq imeeleza kuwa imefaanikiwa kumshika msababishi wa miripuko ya Kadhimain na Jakuk.

Ripoti ya Al-Bayyina Al-Jadidah imeeleza kwamba: Adnan Al-Asadi msaidizi wa Wizara ya Upelelezi ya Iraq alieleza kuwa; Wizara ya Upelelezi ya Iraq imefaanikiwa kumtambua msababishi wa miripuko ya Kadhimain na Jakuk na kumtia mbaroni mtu huyo.

Akiendelea kusema: Miripuko hiyo ilikuwa imeshaandaliwa na watu hao na kuweka mabomu katika magari na kusababisha kuuwa watu wasokua na hatia katika Mkoa wa Kadhimain.

Aidha katika Eid Al-Udh`ha kulitokea miripuko kadhaa katika Mkoa wa Kadhimain na kuuwa mamia ya watu katika Mkoa huo.