21 Novemba 2012 - 17:25

Rais wa Jamuhuri ya Misri Muhammad Mursi alieleza kua uovu na unyama unaofanywa na Israel utaisha leo hii.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Muhammad Mursi rais wa Jamuhuri ya Misri alieleza kua maongezi ya pande mbili baina ya Palestina na Israel itafahamika leo, na tija yake baada ya masaa kadhaa.

Shirika la habari la As-Sharq Al-Ausat la Misri aidha limenakili maneno ya rais wa nchi hiyo akisema: Uovu na unyama unaofanywa na Israel utaisha leo hii.

Kulingana na ripoti hii, Rais wa Jamuhuri ya Misri baada ya mazishi ya Dada yake katika Mkoa wa Al-Sharqiah mashriki mwa Cairo alisema: Maonyesho ya kuchekesha ya Israel Ghaza yataisha leo hii.

Aidha alisisitiza kwa kusema: Maongezi ya pande mbili baina ya Palestina na Israel itafahamika leo, na tija yake itakua baada ya masaa kadhaa na kuleta matunda mazuri.