shirika la Habari la Ahlul Bayut(a.s)-ABNA: Ally Akbar Swalehiy, waziri wa mambo ya nje y a Iran katika mkutano huo alimkabidhi Rais wa Misri barua kutoka kwa Ahmad Najad Rais wa Iran.Vyombo vya habari vya Misri baada ya kutangaza habari hiyo ya mkutano huo, Muhammad Kaamil Amru, waziri wa mambo ya nje wa Misri pia alikuwepo katika mkutano huo ambapo walizungumzia hali halisi ya mashariki ya kati ikiwemo hali mbaya iliopo nchini Syria.Swalehiy baada ya kufika mjini Cairo asubuhi ya leo kabla ya mazungumzo yake na Mursiy alikutana na Nabil Arabiy mkuu wa umoja wa waarabu na Ahdhar Ibrahim wakili wa umoja wa mataifa katika masuala ya Syria.
9 Januari 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 380429
Vyanzo vya habari vyaarifu kuwa waziri wa mambo ya nje ya Iran akutana na Rais wa Misri katika ikulu ya nchi hiyo