Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Shirika la IAEA Ali Asghar Soltanieh amesema pande mbili zitajadili mapendekezo mapya katika mkutano unaofuata. Kwa mujibu wa Shirika la habari la Iran FRAS, Bw Soltanieh amesema katika mazungumzo ya jana baadhi ya tofauti ziliondolewa, na pande mbili zilifikia baadhi ya makubaliano. Wakati huo huo mkuu wa Shirika la nishati ya Atomiki la Iran Bw Fereidoon Abbasi ametangaza kuwa Iran inaendelea kuweka mashinepewa mpya katika kituo cha Nantaz.
13 Februari 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 390920
Duru ya pili ya mazungumzo kati ya Iran na Shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA ilimalizika jana mjini Tehran kuleta maatunda mema baada ya makubaliano baina ya Iran na IAEA.