10 Agosti 2013 - 19:30
Watu 60 wauawa katika shambulizi la mabomu Iraq

Zaidi ya watu 60 wameauawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika wimbi la mashambulizi ya mabomu katika sehemu tofauti nchini Iraq.

 Katika tukio la kwanza, magari 12 yaliyokuwa yametegwa mabomu yalilipuka mjini Baghdad na kuwaua zaidi ya watu 30 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100 wakati watu walipokuwa wakisherehekea kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Katika tukio la pili, watu 5 waliuawa na wengine 18 kujeruhiwa baada ya magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kulipuka katika eneo la Shaab kaskazini mashariki mwa Baghdad. Kwingineko watu 4 waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya gari lililokuwa na mabomu kulipuliwa katika mji wa Kadimiya kaskazini mwa Baghdad. Katika mji wa Kaskazini wa Tuz Khurmatu, watu 11 waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika shambulizi la mabomu lililofanywa karibu na msikiti wa madhehebu ya kishia mjini humo. Mashambulizi hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika mwezi mtukufu wa Ramadhan katika miaka ya hivi karibuni. Mwezi Julai, zaidi ya wairaqi 1000 waliuawa kutokana na machafuko nchini humo.