20 Septemba 2013 - 19:30
Syria yawasilisha ripoti ya silaha za kemikali

Baada ya kuwasilishwa ripoti ya wachunguzi wa silaha za kemikali wa umoja wa mataifa ni Syria nayo yawasilisha ripoti yake ya matumizi ya silaha za kemikali.

Ripoti ya ABNA- Msemaji wa shirika la kupiga marufuku silaha za kemikali amesema Syria imewasilisha ripoti ya silaha za kemikali, na inatarajia kuwasilisha nyaraka nyingine baadaye. Hivi sasa mamlaka ya shirika hilo inatafiti takwimu mbalimbali kwenye ripoti hiyo.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa ambaye anaunga mkono makundi ya upinzani nchini Syria, amesema Ufaransa huenda ikayapatia silaha makundi ya upinzani nchini Syria.

Wizara ya mambo ya nje ya Syria imetoa taarifa ikilaani baadhi ya nchi za Afrika kwa kufadhili na kuyapatia silaha makundi yanayohusiana na kundi la Al-Qaeda nchini Syria ili yapambane na jeshi la serikali. Taarifa hiyo imesema vitendo vya nchi hizo zinakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu vita dhidi ya ugaidi.