Alisema hayo alipohojiwa hivi karibuni na televisheni ya taifa ya Syria Rais Assad alisema makundi ya upinzani nchini Syria yenye silaha si makundi ya upinzani, bali ni makundi ya kigaidi, na yanafanya vitendo vya uharibifu, mauaji makubwa na ya kisirisiri, kama ni nchi nyingine yoyote duniani, pia itayachukua kuwa ni makundi ya kigaidi, badala ya makundi ya upinzani. Rais Assad alisisitiza kuwa, serikali ya Syria itafuata azimio lililopitishwa hivi karibuni na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Syria.
Habari nyingine zinasema mwanachama muhimu wa kundi moja kubwa la upinzani nchini Syria Bw. Safwan Akkasheh aliwaambia waandishi wa habari kuwa, azimio hilo litapunguza sihala za kemikali nchini Syria, na hivyo kupunguza idadi ya vifo na majeruhi ya watu nchini humo.