Mkuu wa majeshi nchini General Prayuth Chan-ochaThailand ametangaza mapinduzi , akisema jeshi sasa linachukua udhibiti wa serikali.
Majeshi yalizingira eneo la tukio mjini Bangkok ambapo makundi ya kisiasa yamekuwa yakifanya mazungumzo kwa siku ya pili na kuwachukua viongozi wao.
Mapinduzi haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa na badala yake jeshi kuchukua mamlaka ya nchi.
Thailand imekabiliwa na mzozo wa kugombania madaraka tangu kaka yake Bi Yingluck , Thaksin Shinawatra, kung'olewa madarakani na jeshi kama waziri mkuu mapema mwaka 2006.
22 Mei 2014 - 15:45
Msimbo wa Habari: 610593
Mkuu wa majeshi nchini Thailand ametangaza mapinduzi , akisema jeshi sasa linachukua udhibiti wa serikali.